Thursday 11 February 2016

Mourihno Sasa Kuinoa Man United ?

Mourihno Sasa Kuinoa Man United ?

Tarehe February 10, 2016
Jose Mourinho
Jose Mourinho
Taarifa nchini Uingereza katika magazeti kadahaa zimedokeza kuwa Jose Mourihno tayari amemalizana na klabu hiyo kwa lengo la kuinoa.
Taarifa hizo zimekuja Muda mfupi baada ya taarifa kuzagaa kwamba boss wa Spurs Mauricio Pochettino huenda akachukua kibarua cha ukocha kwenye klabu ya Manchester United
The Sun linasema Man United wapo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa manager wa Spurs lakini kiuhalisia inasemekana kocha huyo hana wakala.
Pia baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa kocha huyo tayari ameshawaambia marafiki zake kwamba yeye ni kocha wa Man United kuanzia majira ya joto ya jayo.
Tangu kocha huyo atimuliwe na klabu yake ya zamani Chelsea, ripoti za Mourinho kuchukua mikoba ya Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu zimezagaa Ureno, Italia, Hispania na sasa England.

clouds stream