Thursday 11 February 2016

Chui Asababisha Shule 129 Kufungwa Bangalore

Chui Asababisha Shule 129 Kufungwa Bangalore

Tarehe February 11, 2016
chui
Tukio lililotokea Jumapili ambapo chui alivamia chuo mjini Bangalore
Serikali ya jimbo la Bangalore imeagiza kufungwa kwa shule 129, zikiwemo 53 za serikali baada ya chui kuripotiwa kuonekana viungani mwa mji wa Bangalore.
Afisa mkuu wa huduma za wanyamapori jimbo la Karnataka, Ravi Ralph amesema wakazi wa mji huo wametakiwa kutotoka nje kwa sababu ya usalama wao. Polisi na maafisa wa misitu wanaendelea kumsaka mnyama huyo.
Mapema jumapili, chui dume aliingia katika shule moja na kuwajeruhi watu sita waliojaribu kumkamata.
Mwanasayansi na mfanyakazi wa idara ya misitu ni miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye operesheni ya kumdhibiti mnyama huyo iliyodumu saa 10.
Sensa ya karibuni zaidi ilionesha kuna karibu chui 14,000 nchini India.

clouds stream