Tuesday 23 February 2016

Nkurunzinza Akubali Mazungumzo Na Wapinzani

Nkurunzinza Akubali Mazungumzo Na Wapinzani

Tarehe February 23, 2016
Rais wa BurundI, Pierre Nkurunzinza (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon (kulia).
Rais wa BurundI, Pierre Nkurunzinza (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon (kulia).
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amekubali kufanya mazungumzo na upinzani ili kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea katika nchi hiyo.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-moon amesema kuwa rais Nkurunziza ameitikia mwito wa mazungumzo ya upatanishi yanayolenga kumaliza miezi 10 ya mzozo wa kisiasa.
Ban Ki-Moon ambaye yuko mjini Bujumbura katika ziara maalum amesema kuwa rais huyo pia amekubali kuwaachilia huru wafungwa 2000 huku mamia ya watu wameuawa katika makabiliano baina ya vyombo vya dola na wafuasi wa upinzani.
Machafuko yalianza mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania awamu ya 3 ya urais katika uchaguzi mkuu.
Wapinzani wake walidai kuwa rais huyo alikuwa anakiuka katiba ya nchi inayomtaka kiongozi asitawale kwa zaidi ya vipindi viwili.
Nkurunziza naye anashikilia kuwa hakuchaguliwa wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wake uliofuatia mazungumzo ya kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu lakini mbili na nusu wametorokea mataifa jirani.

clouds stream