Thursday 11 February 2016

Soma Alichonunua Mmiliki Wa Arsenal

Soma Alichonunua Mmiliki Wa Arsenal

Tarehe February 11, 2016
Stan Kroenke
Stan Kroenke
Mashabiki wa Arsenal kwa mda mrefu wamelalamika kuhusu kushindwa kwa kilabu hiyo kununua wachezaji wazuri kila dirisha la uhamisho linapokuwa wazi.
Lakini mwana hisa mkuu katika kilabu hiyo Stan Kroenke amenunua shamba kubwa la ng’ombe lililogharimu pauni milioni 500.
Shamba hilo limepitia kaunti sita na Kroenke ambaye ana thamani ya pauni bilioni 5,sasa anamiliki zaidi ya ekari 865,000 za ardhi nchini Marekani,ikiwa ni eneo lililo mara tatu zaidi ya ukubwa wa mji wa Los Angeles,na mara nne na nusu ya ukubwa wa mji wa New York.
Mtu tajiri zaidi nchini India Mukesh Ambani amefanya hivyo na amefanya hivyo kwa mtindo,Mukesh mwenye umri wa miaka 58 ambaye ndio mwanzilishi wa Cricket Franchise Mumbai Indians ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 alijenga jumba refu lenye ghrofa 27,na futi 400,000 mraba mjini Mumbai.
Likiwa na thamani ya dola bilioni ,jumba hilo kwa jina Antilla limedaiwa kuwa jumba ghali duniani,Ni nani asiyetaka ghorofa sita za chini ya ardhi za kuegesha magari,maeneo matatu ya kuegesha ndege na wafanyikazi 600?.

clouds stream