Friday 5 February 2016

Majeraha Yamuweka Nje Rosicky Kwa Miezi Mitatu

Majeraha Yamuweka Nje Rosicky Kwa Miezi Mitatu

Tarehe February 5, 2016
Tomas Rosicky
Tomas Rosicky
Kiungo wa kati wa kilabu ya Arsenal Tomas Rosicky hatochezea timu yake kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kandarasi yake inakamilika katika msimu wa joto,alipata jeraha jingine la paja wakati wa mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi baada ya kipindi cha miezi saba akiuguza jereha,Mchezaji huyo wa taifa la Czech alijiunga na Arsenal mnamo mwezi Mei mwaka 2006.
Alipoulizwa iwapo Rosicky ameichezea Arsenal mechi yake ya mwisho,Wenger alijibu:Natumai hapana ,lakini jeraha hilo ni baya sana.Rosicky ambaye aliichezea Arsenal mara 246 alisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu uliopita.
Wakati huohuo,Wenger amethibitisha kwamba mshambuliaji Danny Welbeck atarudi kuwachezea wachezaji wa Arsenal wasiozidi umri wa miaka 21 siku ya ijumaa.
Mchezaji huyo wa Uingereza,mwenye umri wa miaka 25,ameuguza jereha tangu mwezi Aprili 2015 baada ya kupata jeraha hilo katika mechi iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea.

clouds stream