Thursday 10 March 2016

Dr. Shein Uso Kwa Uso Na Maalim Seif

Dr. Shein Uso Kwa Uso Na Maalim Seif

Tarehe March 10, 2016
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Maalim Seif jijini Dares salaam.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Maalim Seif jijini Dares salaam.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein jana amemjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali.
Aidha, Dr.Shein aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Dkt. Mwinyihaji Makame.
Kwa upande wake Maalim Seif alimwambia Dr. Shein kuwa  afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku.
Dr. Shein na Maalim Seif ndio wagombea urais wenye upinzani  mkubwa Visiwani Zanzibar ambapo Chama cha CUF kimetangaza kususia Uchaguzi wa marudio huku chama cha Mapinduzi(CCM) kikiwataka wanachama wake kujiaandaa kwa ajili ya uchaguzi huo. Utakaofanyika machi 20.

clouds stream