Friday 4 March 2016

Saa Za Kisasa Zitumiwazo Kufanya Udanganyifu Katika Mitihani

Saa Za Kisasa Zitumiwazo Kufanya Udanganyifu Katika Mitihani

Tarehe March 4, 2016


160304101302_cheating_watch_640x360__nocredit
Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani. Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.
Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba ya data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha, zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na badala ya kuonesha kilichomo ndani ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa.
Mojawapo ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB wakati  nyingine ambayo inatarajiwa kuanza kuuzwa baadaye mwaka huu  itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi hata video.
Baadhi ya saa hizo  zina kifaa kidogo sana cha kusikilizia na hakitumii nyaya (wireless) jambo linalomwezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila ya kuonekana.
Naibu Mwalimu Mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza zikawashawishi wanafunzi kudanganya katika mtihani.
Amesema ingawa saa hizo zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta katika vyumba vya mitihani, bado ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani hivyo uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.

clouds stream