Thursday 17 March 2016

Magufuli Aitumbua IPTL , Ataka Ndoa Yake Na TANESCO Ife


Magufuli Aitumbua IPTL , Ataka Ndoa Yake Na TANESCO Ife

Tarehe March 16, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL iliingia mkataba wa hovyo na Serikali na hivyo Serikali yake haitaendelea nao.
Rais John Magufuli amesema hayo leo wakati akizindua ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa Megawati 240 cha Kinyerezi II Jijini Dar es salaam ambapo katika kipindi cha siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani kampuni hiyo tayari imeshalipwa kiasi cha shilingi Bilioni 36.
Kampuni hiyo ya IPTL ambayo inamilikiwa na Habirnder Seth Singh inalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) shilingi milioni 40 hadi shilingi milioni 104 kwa siku kama gharama ya kuuziana umeme kati ya kampuni hizo mbili.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo Joseph Makandege, malipo hayo yanahusisha gharama za uwekezaji ambazo ni senti mbili kwa unit moja ya umeme na senti 28  kama gharama za uzalishaji.
Amesema “IPTL inaiuzia TANESCO zaidi ya megawati 85 kwa siku na malipo yote yanakatwa kodi ya Ongezeko la Thamani yaani VAT.
Naye Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe hivi karibuni alimtaka Rais Magufuli kumaliza kile alichodai kuwa ni ufisadi wa TANESCO wa kuilipa kampuni hiyo kiasi hicho kikubwa cha fedha ambapo ni takribani bilioni 36 zimeshalipwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani.
Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini.

clouds stream