Thursday 10 March 2016

Simba Kukaa Kileleni Leo?

Simba Kukaa Kileleni Leo?

Tarehe March 10, 2016
Hamis Kiiza wa Simba akishangilia
Kama Simba itashinda leo dhidi ya Ndanda Fc bila shaka itakua imeshika usukani wa wal ligi kuu ya Vodacom.
Simba wanaikaribisha Ndanda leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakihitaji ushindi ili kuongoza ligi.
Na kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba timu yake ipo vizuri baada ya maandalizi ya tangu Jumatatu wakiwa kambini nje kidogo ya mji ili wachezaji wapate utulivu.
Ikumbukwe Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 48, baada ya kucheza mechi 21, ikiizidi pointi moja Azam FC iliyo nafasi ya tatu na ikizidwa kwa mbili na vinara, Yanga.

clouds stream