Monday 14 March 2016

Jinsi Makonda Alivyomng’oa Meck Sadick Dar Es Salaam

Jinsi Makonda Alivyomng’oa Meck Sadick Dar Es Salaam

Tarehe March 13, 2016
Bw. Paul Makonda (kushoto) pamoja na Bw. Mek Sadick.
Bw. Paul Makonda (kushoto) pamoja na Bw. Mek Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Paul Makonda leo ameteuliwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam  na kumuhamisha  Said Meck Sadick  kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
Aidha, Makonda hivi karibuni amejizolea umaarufu kufuatia kufanikiwa kuwasafirisha walimu bure kwenye daladala mpango ulioanza wiki iliyopita licha ya kukumbwa na Changamoto kadhaa ikiwemo walimu kubughuziwa na makondakta.
Licha ya kuwasafirisha walimu bure Makonda amekuja wazo jipya lingine  lijulikanalo kama mtaa wa baa hii ni  kufuatia Wilaya ya Kinondoni kugubikwa na baa  katika maeneo  mengi  ikiwemo jirani na misikiti na  Makanisa.
Mpango huo ni maalumu kwa ajili za kuziweka baa zote sehemu moja ili kuepusha bughuza kwa watu wengine wasiojihusisha na starehe mbalimbali zinazopatikana kwenye baa hizo.
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi mara baada ya kupata taarifa ya Makonda kuteuliwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wamesema huenda Rais Magufuli amemteua   kutokana na ubunifu wake uliopelekea kumzidi kete Bw. Meck Sadick.

clouds stream