Friday 11 March 2016

Maalim Seif Akana Kuzungumza Siasa Na Shein

Maalim Seif Akana Kuzungumza Siasa Na Shein

Tarehe March 12, 2016
1
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein alipomtembelea Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Hamad
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Hamad amesema mikutano yake ya hivi karibuni na Rais wa Tanzania John Magufuli na yule wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein haikua na agenda yoyote ya kujadili hali ya siasa inayoendelea visiwani Zanzibar.
Maalim Seif ameyasema hayo baada ya kuwepo na tetesi kuwa ugeni wa maraisi hao ulilenga kuzungumzia uchaguzi wa marudio wa Zanzibar  ambao utafanyika Machi 8 mwaka huu.
Alisema Rais Magufuli na Shein  walikwenda kumjulia hali kibinadamu tu hivyo kuwataka wazanzibari na wafuasi wa CUF kutokuwa na hofu yoyote.
Ikumbuke kwamba CUF imegomea uchaguzi wa marudio Zanzibar  ikishinikiza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  itangaze mshindi wa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Maalim Seif amepumzishwa katika hospitali ya Serena baada ya kuugua akiwa safarini kutoka Zanzibar  kwenda Dar es Salaam.

clouds stream