Tuesday 22 March 2016

Mkuu Wa Wilaya Amuomba Rais Magufuli Asimteue Katika Nafasi Hiyo

Mkuu Wa Wilaya Amuomba Rais Magufuli Asimteue Katika Nafasi Hiyo

Tarehe March 22, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais Dkt. John Magufuli asimteue katika orodha ya Wakuu wa Wilaya wapya anaotarajiwa kuwateua hivi karibuni kwa madai kuwa anahitaji apate fursa zaidi ya kusimamia biashara zake zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya Ukuu wa Wilaya.
Mayenga aliweka wazi ombi hilo kwa Rais Magufuli hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika kikao cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mkoani Shinyanga ikiwa ni siku chache tu tangu Rais Magufuli aweke bayana vigezo vitakavyotumika katika kuwateua wakuu wa wilaya.
“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi ili isitafsiriwe kwamba nimeogopa lasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano lakini nimeona ni vyema nibakie na ubunge na biashara zangu,” amesema Mayenga ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM).
Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

clouds stream