Monday 14 March 2016

Rais Magufuli Apanga Safu Ya Wakuu Wa Mikoa, Sura Mpya 13, Makonda Achukua Dar Es Salaam.

Rais Magufuli Apanga Safu Ya Wakuu Wa Mikoa, Sura Mpya 13, Makonda Achukua Dar Es Salaam.

Tarehe March 13, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wakihamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Akitangaza uteuzi huo, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe Ikulu Jijini Dar es Salaam, amesema Wakuu wa Mikoa walioteuliwa na Rais ni kama ifuatavyo.
Mh. Paul Makonda (Dar es Salaam), Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga (Geita), Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (Kagera), Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga (Katavi), Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma), Mh. Godfrey Zambi (Lindi), Dkt. Steven Kebwe (Morogoro), Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven (Rukwa), Mh. Anna Malecela Kilango (Shinyanga), Mhandisi Methew Mtigumwe (Singida), Mh. Antony Mataka (Simiyu), Mh. Aggrey Mwanri (Tabora), Mh. Martine Shigela (Tanga), Mh. Jordan Mungire Rugimbana (Dodoma), Mh. Said Meck Sadiki (Kilimanjaro), Mh. Magesa Mulongo (Mara), Mh. Amos Gabriel Makalla (Mbeya).
Wengine ni Mh. John Vianey Mongella (Mwanza), Mh. Daudi Felix Ntibenda (Arusha), Mh. Amina Juma Masenza (Iringa), Mh. Joel Nkaya Bendera (Manyara), Mh. Halima Omary Dendegu (Mtwara), Dkt. Rehema Nchimbi (Njombe), Mhandisi Evarist Ndikilo (Pwani), Mh. Said Thabit Mwambungu (Ruvuma) na Luteni Mstaafu Chiku Galawa (Mkoa Mpya wa Songwe).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wakuu wote wa Mikoa wataapishwa Machi 15, 2016 siku ya Jumanne saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

clouds stream