Friday 11 March 2016

Mabomu Yatikisa, Wateja Wakizua Tafrani Benki Ya CRDB Mbagala

Mabomu Yatikisa, Wateja Wakizua Tafrani Benki Ya CRDB Mbagala

Tarehe March 11, 2016
Askari kutoka jeshi la Polisi.Sio picha halisi ya tukio la Mbagala.
Askari kutoka jeshi la Polisi. (Sio picha halisi ya tukio la Mbagala.)
Wateja watatu wamezua tafrani ndani ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala leo kufuatia kukiuka sheria za Benki zinazokataza wateja  kuongea na  simu ndani ya Benki  ambapo Polisi walilazimika kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu waliojikusanya mbele ya Benki hiyo kutazama seke seke hilo.
Inadaiwa kuwa  mtu mmoja alikuwa akiongea na simu na wengine  wawili waki-chat   ndani ya benki hiyo suala ambalo ni kinyume na taratibu  ambapo Mlinzi wa Benki hiyo aliwataka kuacha kufanya hivyo lakini walikaidi maagizo hayo.
Baada ya mlinzi kuona hivyo alitoa taarifa kituo cha polisi Mbagala – Maturubai, na  polisi, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishano baada ya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza kupigana nao hali iliyopelekea watu kuanza kujaa kutazama  huku Polisi wakilazimika kuwatawanya kwa mabomu na kuondoka  na wateja hao.

clouds stream