Tuesday 22 March 2016

UKAWA Yaibuka Kidedea Uchaguzi Meya Jiji La Dar Es Salaam

UKAWA Yaibuka Kidedea Uchaguzi Meya Jiji La Dar Es Salaam

Tarehe March 22, 2016
tanzania2011_0106_dar_askarimonument
tanzania2011_0106_dar_askarimonument
Diwani Isaya Mwita kupitia Vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es salaam baada ya kuishinda CCM iliyopata kura 67, huku UKAWA wakipata kura 84, ambapo kura 7 ziliharibika.
Uchaguzi huo ulifanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Uchaguzi huo uliahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM likidaiwa kutolewa na Mahakama Hakimu Mkazi wa Kisutu.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Magufuli aliingilia kati mvutano wa Umeya katika Jiji la Dar es Salaam na kuwaomba wanachama wa CCM kukubali uchaguzi kufanyika na kwamba yeyote atakayeshinda apewe kwani watanzania hawahitaji chama bali maendeleo bila kujali yanatoka chama gani au upande gani.

clouds stream