Friday 11 March 2016

Paul Scholes Atoa Neno Zito Kwa Man United Soma Hapa


Paul Scholes Atoa Neno Zito Kwa Man United Soma Hapa


Tarehe March 11, 2016
 Paul Scholes
Paul Scholes

Manchester United haifai na haina mipango ili limejidhihirisha katika mchezo wao na Liverpool kwa kuruhusu kufungwa 2-0.
Maneno hayo ameyatoa aliyekuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Paul Scholes ambaye alifuatilia kwa karibu mchezo huo
Daniel Sturridge na Firmino walifunga bao kila mmoja na kudidimiza matumaini ya Manchester United huku David De gea akizuia mashambulio mengi ya Liverpool.
Scholes ambaye aliichezea Manchester United mara 718 aliambia BT Sport kwamba kilabu hiyo ya Old Trafford huwa na viwango fulani lakini kufikia sasa imefeli kuafikia viwango hivyo.
Aliongezea:Liverpool ilikuwa na mpango wa kucheza,Lakini United hawakuwa na mpango wowote,Awamu ya pili ya mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa Old Trafford Alhamisi ijayo.
”Manchester United inafaa kuwania ligi ya Uingereza na kombe la vilabu bingwa”,alisema Scholes.
Wametumia pauni milioni 300 na bado wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi,Wameshushwa hadi katika ligi ya Europa baada ya kushindwa katika kombe la vilabu bingwa.

clouds stream