Wednesday 20 July 2016

Adhabu Kwa Wasaliti CCM Haikwepeki-Kinana


Tarehe July 20, 2016Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema wasaliti wote ndani ya chama watapata adhabu yao kulingana na kiwango cha makosa yao.
Amesema adhabu hizo zitaanzia kwa wale waliokisaliti chama hicho na kusaidia upinzani hasa katika uchaguzi uliopita huku wengine wakiyumba katika misimamo yao na kushindwa kusaidia wengine katika kampeni.
Inaaminika kuwa baadhi ya makada wa chama hicho walitetereka pale aliyekuwa anawania ruhusa ya chama hicho kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa kuamua kung’atuka na kuhamia upinzani baada ya jina lake kukatwa.
Inadaiwa kuwa alipoonda CCM, Mbunge huyo wa zamani wa Monduli na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliacha mtikisiko mkubwa miongoni mwa wanachama kati ya wale waliokuwa wanamkubali na wale wasiomkubali na kuibua mijadala ya ushabiki ndani ya chama hicho hadi kupelekea vigogo wengine kama Makongoro Mahanga na Balozi Mwapachu kujiengua kutoka CCM.
Hatahivyo muda mfupi baada ya uchaguzi kuisha Balozi Mwapachu aliamua kurudi CCM na kudai kuwa alifanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi.
Inaaminika kuwa wapo wengine ambao walitetereka na kukisaliti chama hicho hivyo ni suala la muda tu hadi pale tutakapojua ni nani na nani hasa wametumbuliwa kwa kukisaliti chama tawala.

clouds stream