Friday 15 July 2016

Uchakachuzi Mizani Ya Pamba Wafikisha Saba Kizimbani


Tarehe July 15, 2016cotton
Jumla ya wafanyabiashara 7 wamefunguliwa kesi mahakamani na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) wakituhumiwa kufanya uchakachuaji wa mizani ya kupimia Pamba.
Kesi nne kati ya hizo tayari zimeshatolewa hukumu na wafanyabiashara hao kulipa faini huku zilizobakia zikiendelea kuunguruma mahakamani.
Kaimu Meneja wa Elimu, Habari na Mawasiliano kutoka WMA, Irene John amesema hatua hizo zimefikiwa kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa pamba hususani kanda ya ziwa.
Amesema imezoeleka kila msimu wa Pamba unapofika, wafanyabiashara hao wamekuwa wakitumia mizani zilizochakachuliwa kuwaibia wakulima wa Pamba na ndipo msimu huu ulipoanza wakatuma maafisa wa WMA katika vituo vyote panapouzwa pamba ili kuhakikisha uuzaji wa zao hilo la biashara unafanyika kwa kutumia vipimo sahihi ili kumlinda mkulima.
“Katika ukaguzi huo ndipo wafanyabiashara hao saba wasio waaminifu wakabainika wakitumia mizani zilizochakachuliwa ili kuwaibia wakuliza wa pamba,” amesema.
Hatahivyo amewaasa wakulima hao kuacha mchezo wa kuweka maji, mchanga au mawe ili kupata kilo nyingi pale wanapotaka kuuza pamba yao kwani vitendo hivyo vinaathiri ubora wa pamba na hivyo kupoteza thamani ya zao hilo.

clouds stream