Monday 18 July 2016

BAVICHA, UVCCM Sasa Kuviziana Dodoma


Tarehe July 18, 2016ccm_cdm
ccm_cdm
Ujumbe wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), umetua Mjini Dodoma kwa lengo maalum la kuwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali waliazimia kufanya kila wawezalo ili kuzuia Mkutano Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu amesema kuwa wamefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.
Amesema akiwa Mjini hapo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuratibu shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wao kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki ila cha kushangaza sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA.
“Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” amesema.
Ameongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais, Dkt. John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.
Amewahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu huku akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.
Tayari BAVICHA wametangaza kurudi mjini Dodoma kwa lengo la kufanya Mkutano wao wa Kamati ya Kiutendaji licha ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwataka kusitisha mpango wao wa kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa CCM.

clouds stream