Monday 4 July 2016

UVCCM Waichimba ‘Mkwara’ BAVICHA Kuvuruga Mkutano Wao


Tarehe July 4, 20161
1
Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeonya vikali mpango wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kutaka kuvuruga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam na kudai kuwa watawakabiliana na nguvu zote za BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.
Amesema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya ili kukihami vilivyo chama chao.
CCM inatarajia kufanya Mkutano Mkuu Maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli atakabidhiwa rasmi Uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi wake, Dkt. Jakaya Kikwete.
Wakati huohuo BAVICHA imepanga kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.

clouds stream