Tuesday 26 July 2016

Jeshi La Polisi Lawasaka Wabunge 2 Chadema


Tarehe July 26, 2016Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Willy Qulwi Qambalo, Mbunge wa Karatu.
Wabunge 2 wa Chadema wako matatani kufuatia kuitwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha na kutakiwa kuripoti kwa RCO kufuatia madai ya kufanya mikutano ya kisiasa suala ambalo limepigwa marufuku.
Wabunge walioitwa  kwa mahojiano   ni   mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo na  mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso.
Mwingine aliyeitwa ni  Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Jubilate Mnyenye na  Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta wote   wanadaiwa  kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.
Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.
Parreso alisema, walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane  lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.
Katika hatua nyingine  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.
Marufuku ya mikutano ya kisiasa imeendelea kuvikumba vyama vya Upinzani licha ya Jeshi la Polisi kusema kwamba halijapiga marufuku mikutano hiyo ya kisiasa.

clouds stream