Tuesday 12 July 2016

Makachero Jeshi La Polisi Wamnasa Gwajima


Tarehe July 12, 2016Askofu Josephat Gwajima.
Askofu Josephat Gwajima.
Makachero kutoka Jeshi la Polisi   waliopiga kambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wamefanikiwa kumkamata Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Inadaiwa kuwa baada ya kukamatwa simu zake zimechukuliwa na makachero hao kwa ajili ya uchunguzi kufuatia mahubiri yake yaliyokosoa utendaji wa Rais Dkt.Jakaya Kikwete kanisani kwake Juni 11.
Aidha, Mara baada ya mahubiri hayo Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam lilitangaza kumsaka popote pale alipo huku habari zaidi zikibaninisha kuwa askofu huyo alitimkia ughaibuni hadi jana alipokamatwa akiingia nchini.

clouds stream