Saturday 16 July 2016

Andriy Shevchenko Aula Umeneja Timu Ya Taifa Ukraine


Tarehe July 16, 2016Andriy Shevchenko
Andriy Shevchenko
Andriy Shevchenko
Ukraine imemteua mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko kuwa meneja mpya wa timu ya taifa.
Shevchenko, 39, aliyechezea timu ya taifa mara 111, atajaza nafasi ya Mykhaylo Fomenko, aliyeondoka baada ya taifa hilo kuondolewa michuano ya Euro 2016 katika hatua ya makundi.
Shevchenko alikuwa msaidizi wa Fomenko Ukraine waliposhindwa mechi zao zote dhidi ya Ujerumani, Ireland Kaskazini na Poland.
Mchezaji huyo wa zamani wa Dynamo Kyiv, aliyestaafu mwaka 2012, hajawahi kuhudumu kama meneja awali.

clouds stream