Saturday 16 July 2016

Vigogo 3 Jeshi La Polisi Wang’oka Sakata La Mishahara Hewa



Tarehe July 16, 2016jeshi-la-polisi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya malipo hewa  ya  posho ya chakula (Ration Allowance) kwa watu ambao sio askari.
Hatua hii ni mwendelezo wa uchunguzi wa tuhuma za kufanya malipo hewa ya kiasi cha sh. 305,820,000/= zilizopelekea kusimamishwa kazi kwa Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Bw.Frank Charles Msaki wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa kurugenzi ya mawasiliano Wizara ya Mambo ya Ndani imewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni;
(i)Bw. Damian Aloys Bupamba ambaye ni Mhasibu Daraja la II
(ii) Bi, Ida Dennis Moyo Mhasibu Daraja la I kwa makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
(iii) Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Milambo Mwita Milambo kwa makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Watumishi wote watatu  wanadaiwa  wamehusika kufanya malipo hayo  jambo ambalo ni kinyume na Kanuni F.9 ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995 kama zilizovyorekebishwa mwaka 2013.
Katibu Mkuu amewasimamisha wahusika hao ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma dhidi yao unaofanyika kufuatia Uchunguzi Maalamu wa Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi uliobaini makosa ya malipo hewa.

clouds stream