Monday 25 July 2016

Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Septemba, Mawaziri Wengine Kufuata


Tarehe July 25, 2016Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote  hapa nchini kuhakikisha kuwa wanahamia makao Makuu ya Dodoma kama amri ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoitoa kwenye mkutano maalumu wa CCM.
Akizungumza kwenye maadhimisho  ya Mashujaa Kitaifa, yaliyofanyika mjini Dodoma Mhe Majaliwa amesema baada ya agizo la Rais alimuita Waziri wa nchi ofisi  ya Waziri mkuu pamoja na Katibu mkuu na kuwaagiza wakamilishe nyumba yake atahamia mwezi wa tisa mkoani Dodoma.
Amesema yeye akitangulia Dodoma mwezi wa tisa Mawaziri wengine wote wamfuate ikiwa ni kutii agizo la Rais Magufuli linalowataka watendaji wa serikali kuhamia Dodoma.
Amewasihi wana Dodoma kuwa serikali inafika Dodoma na kusisitiza kuwa utekelezaji wake anausimamia kwa nguvu zote.
Ametoa nasaha kwa wananchi kuhakikisha kuwa Dodoma inakuwa ni kisiwa cha amani, kuongeza uwekezaji katika mahoteli, Nyumba za kulala wageni na huduma nyingineno  kwa kuwa wageni wengi watafika mkoani humo kupata huduma mbalimbali za kiserikali.

clouds stream