Thursday 21 July 2016

JK Arusha ‘Dongo’ Kwa Waliodhani CCM Ingemfia Mikononi



Tarehe July 21, 2016
Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM anayeondoka katika wadhifa huo, Dkt. Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM, Mjini Dodoma.
Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM anayeondoka katika wadhifa huo, Dkt. Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC), Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayeondoka madarakani, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amerusha dongo kwa wale wote waliofikiria kuwa chama hicho kingemfia mikononi mwake.
Kikwete ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua na kuongoza kikao chake cha mwisho kama Mwenyekiti cha Kamati Kuu (CC) na kuwakebehi wale wote waliodhani kuwa chama hicho kingeanguka kipindi cha uongozi wake.
Amesema waliodhani CCM ingekufa katika uongozi wake na kujiandaa kutoa salamu za rambirambi, basi imekula kwao.
“Wapo wale waliodhani kwamba wangeibuka lakini hawakuibuka na kamwe hawataibuka,” Amesema Dkt. Kikwete.
Wanachama wa CCM wapo Dodoma katika Mkutano Maalum utakaofanyika Julai 23, mwaka huu huku Rais, Dkt. John Magufuli akitarajiwa kuchukua hatamu ya uongozi wa CCM Taifa akimpokea Dkt. Kikwete.

clouds stream