Saturday 16 July 2016

Hizi Ndizo Shule 10 Bora Na Shule 10 Za Mwisho




Tarehe July 16, 2016Shule ya Sekondari Kisimiri.

Shule ya Sekondari Kisimiri.
Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) leo limetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016 ambapo  Imezitaja shule kumi zilizofanya vizuri huku shule ya sekondari ya serikali ya Kisimiri ikiongoza kwa matokeo hayo.
Licha ya shule  kumi bora Necta imezitaja shule kumi zilizofanya vibaya katika matokeo huku asilimia kubwa ya shule hizo zimetokea visiwani Zanzibar.
Aidha, Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi(Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7.
Necta imebainisha kuwa  upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:
Shule 10 Bora Kitaifa
  1. Kisimiri (Government)
  2. Feza Boys (Private)
  3. Mwanza Alliance Girls (Private)
  4. Feza Girls (Private)
  5. Tabora Boys (Government)
  6. Marian Boys (Private)
  7. Kibaha (Government)
  8. Mzumbe (Government)
  9. Ilboru (Government)
  10. Tandahimba (Private)
Shule 10  za  Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)
2.Ben bella ( Unguja)
3.Tumekuja (Unguja)
4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)
5.Jang’ombe (Unguja )
6.Kiembesamaki (Unguja )
7.Tanzania Adventist ( Arusha )
8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )
9.Azania (Dar es salaam )
10: Lumumba (Unguja)

clouds stream