Sunday 31 July 2016

Lembeli Ajitosa Mkutano Wa Rais Magufuli Shinyanga

Tarehe Aug 01, 2016
Raqis Magufuli na James Lembeli.
Rais Magufuli na James Lembeli.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama, James Lembeli ameibuka katika Mkutano wa Rais, John Pombe Magufuli uliofanyika Mjini Kahama baada ya Rais Magufuli kumkaribisha na kumtaka arudi Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lembeli aliihama CCM na kuhamia CHADEMA mwaka jana na kugombea Ubunge Jimbo la Kahama na kuangukia pua.
Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi CCM na kusema kuwa kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza kitu, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.
Naye Lembeli amesema amekwenda katika mkutano huo kwa kuwa kazi inayofanywa na Rais Magufuli ndiyo ambayo amekuwa akiipigania alipokuwa Mbunge wa Kahama kwani rushwa imekithiri.
Aidha amerudia kauli yake aliyoitoa siku chache zilizopita na kusema kuwa hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama hicho akisafishe kabisa.

clouds stream