Monday 25 July 2016

Zitto Kushuhudia Hillary Clinton Akithibitishwa Mgombea Wa Democratic

Tarehe July 25, 2016Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe.
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameondoka nchini kuelekea Philadelphia nchini Marekani kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention) utakaomthibitisha Bi.Hillary Clinton kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis, akiwa kwenye Mkutano huo Zitto atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani pamoja na kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la Wanachama wa ACT Diaspora la nchini Marekani.

Aidha, pamoja na mambo mengine Zitto atakuwa na mazungumzo maalum na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad juu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar na Taifa kwa Ujumla.
Zitto na Maalim Seif ndio wanasiasa pekee nchini walioalikwa kwenye shughuli za chaguzi za nchini Marekani.

clouds stream