Monday 27 June 2016

Afariki Kwa Kunywa Gongo Kupitiliza


Tarehe June 27, 20161 (1)
Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
Mkazi wa Mondo katika Kijiji cha Kitumba wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Juni 23, mwaka huu, saa 8:00 mchana kitongojini humo ambapo alieleza kuwa, baada ya kufika nyumbani kwa Daudi Mtula anayeuza gongo kwa siri, Magola alikunywa pombe hiyo kupita kiasi akaishiwa nguvu na kupoteza maisha.
“Mtu huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,” Kamanda Msangi alisema na kuongeza kuwa, baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka na kuuacha mwili wa marehemu nyumbani kwake.
Msangi alisema kuwa Polisi inamtafuta muuzaji huyo wa pombe kwa ajili ya kumchukulia hatua za kisheria.
Pia alitoa wito kwa wananchi kuiunga Polisi mkono kudhibiti biashara ya pombe hiyo haramu.

clouds stream