Tuesday 14 June 2016

Prof. Lipumba Akataliwa CUF

Prof. Lipumba Akataliwa CUF

Tarehe June 14, 2016Mwenyekiti wa Zamani wa chama cha CUF  Prof . Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa Zamani wa chama cha CUF Prof . Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa Zamani wa chama cha CUF  Prof . Ibrahim Lipumba  aliyetangaza kutengua uamuzi wake wa Kujiuzulu  na kurejea kwenye cheo chake cha  awali  cha Mwenyekiti wa chama hicho, Chama hicho kimemkataa.
Prof. Lipumba ambaye  jana alifika makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam  na wapambe wake alitangaza nia ya kutaka kurejea kwenye cheo chake kufuatia kujiuzulu  Uenyekiti wa  Chama hicho mwaka jana  kutokana na ujio wa Mwanasiasa Edward Lowassa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema haoni chochote cha maana kwa kuwa sababu zilizomuondoa bado zipo, hivyo amehoji kinachomrudisha ni nini?
Naye Twaha Taslima ambaye  ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema Katiba ya Chama hicho hairuhusu Kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake ya awali.
Prof. Ibrahim Lipumba ni Mchumi wa kimataifa  amezaliwa tar. 6 Juni 1952, Ilolangulu, Tabora, Tanzania amewahi kugombea urais mara kadhaa kupitia Chama cha Wananchi CUF.

clouds stream