Sunday 19 June 2016

Lowassa Ailipua NEC, Adai Ni Kitengo Cha CCM


Tarehe June 19, 2016Mwanasiasa Edward Lowassa akiwa katika Maafali ya vijana wa Chadema katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo.
Mwanasiasa Edward Lowassa akiwa katika Maafali ya vijana wa Chadema katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo.
Aliyekuwa  Mgombea  urais kwa tiketi ya Ukawa Edward  Lowassa  amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kupigania   Tume huru ya Uchaguzi kufuatia kutoridhika na matokeo ya Uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka.
Akizungumza kwenye maafali ya Vijana wa Chadema Vyuo vikuu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Lowassa amesema kuwa ili uchaguzi uwe huru na wa Haki ni lazima watanzania wapiganie Tume huru ya Uchaguzi kwa madai kwamba Tume ya sasa ya Uchaguzi ni kama kitengo cha CCM.
Lowassa alisema watanzania wanapaswa kuchukua mfano wa Kenya ambapo wananchi wake wanapigania kuwa na Tume huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi uwe wa haki.
Aliongeza kuwa ni lazima Tume ya Uchaguzi yenye mafungamano na CCM iondoke kwa kuwa imeshindwa kumtangaza mtu aliyeshinda uchaguzi na kusisitiza kuwa kamwe hawezi kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka hata kama ikibidi kufa.
Kwa upande wa ‘Bunge Live’ Lowassa alisema kuwa Bunge kutokuwa Live ni aibu kwa watawala suala ambalo limepelekea  heshima yao kushuka na kupitiliza kwa kuwa kila mwananchi  ana uhuru wa kuapata Habari.
Katika Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 Lowassa  alikuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 6,072,848  sawa  na  asilimia 39.97 nyuma ya Rais Magufuli aliyeshinda kwa kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46.Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wananchama wa Chadema katika maafari hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wananchama wa Chadema katika maafari hayo.Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu chama cha Chadema wakionesha alama ya mabadiliko.
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu chama cha Chadema wakionesha alama ya mabadiliko.

clouds stream