Sunday 19 June 2016

Tetesi Za Soka Ulaya Leo


Tarehe June 19, 2016
Arsen Wenger

Meneja mpya wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili beki wa Italy na Juventus Leonardo Bonucci, 29. (Daily Star Sunday).
Mshambuliaji Wayne Rooney, 30, yuko tayari kusaini mkataba mpya ili astaafu akiwa United (Sun on Sunday).
Mourinho yuko tayari kubadilishana na Chelsea, kwa kuwapa beki Matteo Darmian, 26, ili amchukue kiungo Nemanja Matic, 27. (Sunday People)
Watford wamekataa dau la pauni milioni 25 kutoka Leicester ili kumsajili mshambuliaji Troy Deeney, 27.(Watford Observer)
Manchester City hawataki kutoa pauni milioni 65 wanazotaka Borussia Dortmund kwa ajili ya Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 27.(Manchester Evening News)
City wanataka kumsajili Mshambuliaji wa Celta Vigo na Spain Nolito, 29, kwa pauni millioni 14.1 (Mail on Sunday)
Pep Guardiola pia anajiandaa kutoa pauni milioni 37 kwa Real Madrid ili kumsajili kiungo Toni Kroos, 26.(Sunday Express)
Southampton wanataka pauni milioni 40 kumuuza mshambuliaji kutoka Senegal Sadio Mane, 24, ambaye anasakwa na Liverpool.(Sun on Sunday)
Sunderland wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko na wametoa pauni milioni 11 kwa Roma (Mail on Sunday)
Arsenal wapo tayari kumpa mkataba mpya wa miaka miwili meneja Arsene Wenger, 66, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa (Sunday Mirror)
Chelsea na Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji kutoka Morocco Sofiane Boufal, 22, anayecheza Lille, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona na Atletico Madrid.(Observer)
West Brom na Aston Villa wanataka kumsajili mshambuliaji kutoka Wales, Hal Robson-Kanu, 27, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Reading. (Daily Star Sunday)
Juventus wanataka mmoja kati ya wachezaji watatu watakaoziba pengo la Alvaro Morata, ambaye huenda akaondoka. Wachezaji hao ni Romelu Lukaku, Christian Benteke, na Michy Batshuayi, 22,
Beki wa Liverpool na Slovakia Martin Skrtel, 31, amekubali mkataba wa miaka mitatu Roma. (Emanuele Giulianelli via Sunday Express)
Beki wa Manchester United Daley Blind, 26, ananyatiwa na Arsenal. (Sunday People)
Leicester wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 10 kumtaka beki wa kati wa Burnley Michael Keane, 23. (Mail on Sunday)
Leicester pia wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo Nampalys Mendy, 22, baada ya klabu yake, Nice kukubali dau la pauni milioni 10, Lakini pia wanamtaka kiungo wa Juventus Mario Lemina, 22. (Observer)
Meneja mpya wa Everton Ronald Koeman ameonywa kuwa asifikirie kumtaka Georginio Wijnaldum, wa Newcastle bila ya kuwa na pauni milioni 25 ili kumsajili kiungo huyo (Sunday People)
Manchester United wana wasiwasi kuwa Mshambuliaji wao Marcus Rashford, 18, atachoka
msimu ujao iwapo hatopumzika kipindi hiki (Sun on Sunday)
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

clouds stream