Tuesday 21 June 2016

Magufuli Abariki Kukatwa Kodi Kiinua Mgongo



Tarehe June 21, 2016Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais John Magufuli ametuma ujumbe bungeni kuwa yeye ni mbunge namba moja na anataka mapato yake yote yakatwe kodi stahiki.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitangaza ujumbe huo wa Dk Magufuli kwamba alipewa mapema alipopeleka pendekezo la kukata kodi ya mapato katika kiinua mgongo cha wabunge.
Kwa mujibu wa Dk Mpango, kabla hata ya kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, alipeleka mapendekezo hayo kwa Rais Magufuli ambaye alisisitiza kutoachwa kiongozi yoyote wa serikali katika suala la kodi ya mapato.
“Nataka niwaambie, nilipopeleka hili (kukata kodi kiinua mgongo cha wabunge) kwa Rais, alinishangaa na kisha akasema yeye ni Mtanzania na ni lazima Watanzania wote walipe kodi kwa ajili ya kuendeleza nchi yao,” Dk Mpango aliwaambia wabunge wenzake wakati akifanya majumuisho ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17.
Hatua ya kukatwa kodi katika kiinua mgongo cha wabunge ilizua mijadala mizito baada ya baadhi ya wabunge hao kulalamika kuwa mara nyingi hutumia kiinua hicho kuwasaidia wananchi wao.

clouds stream