Friday 24 June 2016

Makonda Asimamisha Makampuni Ya Ujenzi Wa Barabara Kwa Ubovu Wa Barabara


Tarehe June 25, 20162
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amechukua hatua ya kuzisimamisha na kusitisha kampuni nne za Inshinomya Co. Ltd, Germinex Construction Ltd, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Construction Co. kutokana na ujenzi wa barabara mbovu katika Mkoa wa Dar es salaam.
Mhe. Makonda amechukua hatua hii kutokana na kampuni hizo kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni hayo kutopewa zabuni yeyote katika Mkoa wa Dar es salaam mpaka pale atakapojiridhisha na utendaji kazi kwa makampuni hayo.
Hivi karibuni Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam amekuwa akipigia kelele barabara ambazo zimejengwa chini ya kiwango katika mkoa huo a kuahidi kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha kuwa makampuni yote yanayohusika kwa njia moja ama nyingine na ujenzi wa barabara mbovu yanachukuliwa hatua.

clouds stream