Friday 24 June 2016

ATAKAYEOA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI KUFUNGWA MIAKA 30 JELA

Tarehe:June24,2016

Selikali imewasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2016, unaokusudia pamoja na mambo mengine, kutoa adhabu ya miaka 30 jela kwa mtu yeyote atakayeoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya msingi au ya sekondari.

Adhabu hiyo iko katika marekebisho yanayokusudiwa kufanywa katika Sheria ya Elimu Kifungu cha 60 kinachokusudiwa kufanyiwa marekebisho kwa kuongezewa vifungu vinavyopiga marufuku ndoa kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.unnamed344Kifungu cha 60 A kifungu kidogo cha kwanza ambacho ndio kipya kimeeleza kuwa itakuwa kinyume cha sheria katika mazingira yoyote yale kwa mtu yeyote kumuoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya sekondari au ya msingi.

Kwa mujibu wa kifungu hicho kipya, mtu yeyote atakayekiuka kifungu hicho, sheria hiyo imeweka wazi kuwa atakuwa ametenda kosa na adhabu yake itakuwa kufungwa jela miaka 30.

Sehemu ya tatu ya sheria hiyo imeeleza wazi kuwa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi au wa shule ya sekondari, atakuwa ametenda kosa, ambalo adhabu yake pia ni kwenda jela miaka 30.

Sheria hiyo imekwenda mbali zaidi kwa watu watakaokutwa na hatia ya kushawishi mwanafunzi wa shule ya msingi na shule ya sekondarin aoe au aolewe, wakati akiendelea na shule, naye atakuwa amefanya kosa na adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano, au kwenda jela miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Ili kudhibiti hali hiyo, sheria hiyo imewataka wakuu wa shule na walimu wakuu kutunza taarifa na kuziwakilisha kwa kamishna wa serikali au mwakilishi wake itakayoeleza kwa kina matukio ya ndoa na mimba za wanafunzi na hatua zilizochukuliwa za kisheria dhidi ya waliokutwa na hatia.

Marekebisho hayo ya sheria ya elimu, yamewasilishwa bungeni wiki hii, wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) likiitaja Tanzania kuwa moja ya nchi tatu zinazoongoza kwa ndoa za utotoni.

clouds stream