Sunday 26 June 2016

Serikali Yasitisha Tamko La Utoaji Chakula Muhimbili


Tarehe June 26, 2016Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu.
Serikali imesitisha kwa muda tamko la utoaji vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ili kupisha utafiti wa kina kuhusiana na huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora zaidi kwa watanzania.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba Serikali imeamua kusitisha mpango huo mpaka watakapotangaza tena ili kufanya utafiti zaidi kujua kama kuna faida au hasara kwa wananchi.
“Natoa tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani wananchi,” amesema.
Huduma hiyo ilikuwa inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa ili kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa hao wa kuleta vyakula hospitalini ili kuimarisha afya zao kwa ujumla.
Awali, Hospitali ya Taifa Muhimbili, ilitoa tamko kuwa huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hospitalini hapo kwa shilingi 50,000 ikiwemo shilingi 10,000 ya kumuona daktari, shilingi 10,000 ya kitanda na shilingi 30,000 kwa malipo ya chakula kwa muda wa wiki moja.

clouds stream