Wednesday 29 June 2016

NBS Yakana Kupima UKIMWI Nyumba Kwa Nyumba


Tarehe June 29, 2016BARAZA-1-620x309
BARAZA-1-620x309
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba, ugonjwa wa Ukimwi sasa utapimwa nyumba kwa nyumba.
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo imesema, habari hizo zinatokana na taarifa iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari “Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba”.
NBS imefafanua kuwa ofisi hiyo itafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania kuanzia Septemba 2016 ambapo Ukimwi utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huu.
Utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.
Aidha, katika utafiti huu kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo.

clouds stream