Friday 24 June 2016

Bawa La Ndege Laokotwa Pemba


Tarehe June 24, 2016ClpWnD_WIAE2cUO-e1466722443775
ClpWnD_WIAE2cUO-e1466722443775
Kipande cha ndege kilichookotwa Pemba
Bawa kubwa la ndege ambalo haijafahamika ni la ndege ya shirika gani limeokotwa na wananchi leo katika Bahari ya Hindi kwenye Kisiwa cha Kojani, Pemba.
Bawa la ndege lililopatikana katika bahari ya kisiwa kidogo cha kojani huko kisiwani pemba zanzibar, yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa hicho huku wengi wakiamini ni bawa la ndege ya Malaysia ambayo ilipotea bila kujuilikana hatima yake.
Ndege ya shirika la Malaysia Airlines yenye chapa MH370, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014 haijawahi onekana hadi leo.
Ingawa bado hakuna uhakika ni mabaki ya ndege gani, wataalamu wa usafiri wa anga wameanza hatua ya awali ya uchunguzi wa mabaki hayo ya ndege.

clouds stream