Tuesday 14 June 2016

Polisi Waanza Kuchunguza Sumu Ofisi Ya Meya Mwanza




Tarehe June 15, 2016msangi
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limeanzisha uchunguzi dhidi ya madai ya kupuliziwa hewa ya sumu ofisini kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa jeshi hilo tayari limewahoji watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo lililotokea Juni 13, mwaka huu.
Watumishi wawili wa jiji hilo, katibu muhtasi wa ofisi ya meya, Gladys Chiduo na karani wa ofisi hiyo, Anselemi Mtobesya wameshikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Madai ya sumu kupuliziwa ofisini kwa Meya huyo yaliibuka muda mfupi baada ya kiongozi huyo kuingia ofisini akitoka kwenye ziara ya kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo eneo la Sinai.
Aprili mwaka huu, mstahiki meya Bwire alilazwa katika hospitali moja jijini Nairobi nchini Kenya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kudaiwa kuanguka ofisini kwake.

clouds stream