Sunday 19 June 2016

Saba Wafa, 21 Walazwa Kwa Ugonjwa Usiojulikana Dodoma



Tarehe June 20, 2016ummy mwalimu
waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto, Ummy Mwalimu
Watu sita wa familia moja wamefariki na wengine 21 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana.
Mganga mkuu wa mkoani Dodoma Dkt.James Charles amezungumza kuwa dalili za ugonjwa huo ulioua watu sita na baadhi ya mifugo ni tumbo kuvimba na kujaa maji, kutapika, kuharisha, kupata rangi ya manjano machoni.
Dkt Charles alisema watu wa kwanza kubainika kuugua walikula nyama ya Ng’ombe katika kijiji cha Mwaikisabe.
Akizungumzia ugonjwa huo, waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto, Ummy Mwalimu amesema tayari sampuli zaugonjwa huo zimepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi.
Waziri Mwalimu amewatoa hofu wakazi wa Dodoma walioanza kuhisi kuwa ugonjwa huo ni Kimeta, na kuwataka wasubiri majibu kutoka kwa Mkemia Mkuu.

clouds stream