Thursday 30 June 2016

Magufuli:Tumemkamata Mwizi Wa Milioni 7 Kila Dakika


Tarehe June 30, 2016Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amewaacha wananchi midomo wazi kufuatia kauli yake kwamba serikali imemkamata mtu aliyekuwa akiibia Mamlaka ya Mapato kiasi cha shilingi milioni 7 kila dakika.
Aidha,Rais Magufuli alisema hayo  wakati  akiwaapisha  na kula kiapo cha uadilifu wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya Ikulu jijini Dar es salaam.
“Yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha’”Alisema Rais Magufuli.
Hata hivyo mkuu huyo wa nchi hakuweza kufafanua zaidi kuhusu mtu huyo ambaye bila shaka atakuwa ni  Bilionea kutokana na kuiibia serikali fedha hizo kila dakika ambazo ni jasho la wananchi wanaolipa kodi.

clouds stream