Wednesday 15 June 2016

Basi La Tahmeed Lapata Ajali Mbaya, Lateketea Kwa Moto



Tarehe June 16, 2016Basi la Tahmeed likiteketea kwa moto.

Basi la Tahmeed likiteketea kwa moto.
Ajali mbaya ya Moto imelikumba Basi la Kampuni ya Tahmeed linalofanya safari zake kati ya Tanga- Dar es Salaam ambapo limeteketea lote kwa moto.
Kwa  mujibu wa taarifa za awali zimebainisha kuwa   ajali hiyo imetokea katika  barabara ya Chalinze- Segera, hadi sasa hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiri ndiyo imeteteketea ndani ya basi hilo.
Taarifa hizo  zimeleza kuwa  ajali hiyo  imetokea wakati basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba Msaada akajisaidie (kuchimba dawa) na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya gari na muda mfupi gari lote likashika moto.
13394191_1348476345168087_789764314895306808_n
2

clouds stream