Friday 24 June 2016

Mrema ‘Awageuka’ UKAWA Kufutwa Mikutano Ya Kisiasa


Tarehe June 25, 2016Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Augustine Mrema.
Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Augustine Mrema.
Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Augustine Mrema.
Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amesema kuwa nchi hii haiwezekani kila siku ikawa ni maandamano kwani wananchi wanatakiwa wafanye kazi.
Mrema alisema hayo alipokuwa akizungumzia  kuhusu kauli  ya Rais ya kuzuia mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020  kama haitaviathiri vyama kikiwemo chama anachokiongoza cha TLP.
Mrema alisema  sababu ya kufutwa kwa mikutano hiyo imechangiwa na wapinzani wenyewe kufuatia kususia vikao vya Bunge  na kuitisha mikutano ya kisiasa nchi nzima ikiwa hivisasa wananchi  wanatakiwa kufanya kazi.
”Kwa maoni yangu binafsi hii imetokana na tabia yetu sisi wapinzani kugomea kila kitu hata mambo ambayo yana maslahi kwa taifa, kwa mfano ukiangalia wakati Rais Dkt. John Magufuli anazindua bunge la bajeti wapinzani walimgomea na kutoka nje, hapa walianza kumhukumu kabla hajaanza kazi”- Amesema Mrema.
Kuhusu chama chake kutofanya siasa Mrema amesema yeye hana maandamano ya kila mara hivyo anaamini atakuwa na mikutano halali muda ukifika lakini kwa sasa wananchi wafanye kazi kwanza.

clouds stream