Thursday 16 June 2016

Polisi Wapiga Kambi Kumuwinda Gwajima

Tarehe June 17, 2016Mmoja wa Askari katika nyumba ya Gwajima jijini Dar es salaam.

Mmoja wa Askari katika nyumba ya Gwajima jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Askari katika nyumba ya Gwajima jijini Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda maaulumu ya Dar es salaam limepiga kambi nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kufuatia kutoa kauli ‘tata’dhidi ya Rais Dkt John Magufuli na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kupitia sauti yake iliyoenea katika mitandao ya kijamii imesema kuwa Gwajima  amebaini njama za baadhi ya wanachama wa CCM ambao ‘dili’ zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘flow meter’ ya mafuta yaingiayo nchini na makontena yaliyokamatwa yalikuwa yanawahusu, wameanza kampeni ya chinichini nchi nzima kutaka Rais Magufuli asipewe uenyekiti wa chama hicho.
Sauti ilisema kuwa watu hao wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama wa CCM kuridhia hoja ya kutenga uenyekiti wa chama na urais, ili kumnyima nafasi hiyo Rais Magufuli ambaye utendaji wake umewabana bila kujali ni wa chama chake.
Adiha,Gwajima   amemshauri Rais Magufuli kuwa endapo itatokea hilo, akihame chama hicho na kuendelea na kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Gwajima ambaye amekiri kuwa katika kampeni za Mwaka  alikuwa hamkubali Dkt. Magufuli kutokana na kutokuwa na imani na CCM, amesema amemkubali  sana baada ya kuanza kazi ya urais kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua ndani ya muda mfupi.

clouds stream