Tuesday 14 June 2016

Mrema Bado ‘Anaota’ Cheo Alichoahidiwa Na Magufuli



Tarehe June 14, 201602

Augustine Mrema akiwa na Rais John Magufuli kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya chama cha TLP, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt.  Augustine Lyatonga  Mrema amesema mbali na mambo yote yanayoendelea nchini  bado anaamini Rais wa sasa Dk. John Pombe Magufuli atampa nafasi nono hapo baadae.
Akizungumza na wanahabari leo, Mrema alisema ingawa kwa alikosa ubunge bado anaamini ana nafasi kupata cheo kingine mbali na umri wake kuwa mkubwa na afya yake kuripotiwa kudorora kila mara.
Mrema aliongeza kuwa bado ana uwezo wakuongoza kwani vijana wengi hawajui maadili ya uongozi
“Mimi nitaondoka lakini mahesabu yangu ninayo, Lakini kama nitaondoka sasa hivi nani atawakemea vijana hawa?. Mfano sasa hivi huko Bungeni si munaona. Sisi tutakomaa mpaka vijana wawe na maadili ndio tutawaachia nchi,” alisema Mrema.
Akizungumzia sakata la wabunge wa Ukawa kumsusia spika wa bunge, Dkt Tulia Ackson, Mrema amesema kitendo hicho sio cha kiungwana kwani wabunge hao wameshindwa kuwatumikia vyema wananchi waliowachagua kwa kushindwa kuwasilisha kero zao bungeni.

clouds stream