Tuesday 28 June 2016

Hispania yavuliwa ubingwa

Timu ya taifa ya hispania imeaga michuano ya ulaya baada ya kufungwa na timu ya italia kwa jumla ya mabao mawili bila majibu. Timu ya Hispania ambayo ndio ilikuwa bingwa mtetezi imeaga michuano ya ulaya 2016. Katika mechi hii timu zote mbili zilikuwa zinagombani nafasi ya kucheza robo fainali ya kumbe la ulaya.  Katika dakika ya 33 timu ya Italy ilijipatia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake mahiri Giogrio Chiellini baada ya kipa wa Hispania, De gea kucheza mpira wa adhabu uliopigwa na kisha mchezaji Giogrio Chiellini kuumalizia.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya italia ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

 Lakini katika dakika za lala salama mchezaji Graziano Pelle wa italia aliifungia timu yake ya italia bao la pili, dakika ya 90. Hadi mwisho wa mchezo refa Cuneyt Cakir alipopuliza kipenga cha mwisho, Italia ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.


clouds stream