Friday 10 June 2016

Wadau, Wanaharakati Kumchangia Kijana Aliyemtukana Magufuli



Tarehe June 11, 20161
1
Wadau na wanaharakati wa siasa mjini Arusha wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana Isaack Habakuki aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.
Kijana Habakuki alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa na mahakama kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.
Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000 ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.
“Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema Nanyaro.

clouds stream