Friday 24 June 2016

Cameroon Ajiuzulu Uwaziri Mkuu Wa Uingereza


Tarehe June 24, 201648094743.cached
48094743.cached
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron ametangaza atajiuzulu baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza kubaki katika muungano wa Ulaya (EU).
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya ofisi yake jijini London, Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atabaki ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo ang’atuke.
Cameron ambaye aliongoza kampeni ya kubakia katika muungano wa EU amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Jana raia zaidi ya asilimia 52 walipiga kura za kuitoa nchi ya Uingereza katika Muungano wa Ulaya (EU).
Bwana Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa lina ufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

clouds stream