Monday 20 June 2016

Muhogo Waua Watatu Morogoro


Tarehe June 20, 2016mihogo ya kuchemsha
mihogo ya kuchemsha
Watu watatu wamekufa mkoani Morogoro na wengine wawili kunusurika kifo, kutokana na kula muhogo wa kuchemsha unaosadikiwa una sumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema tukio hilo lilitokea Juni 18, mwaka huu saa 9 alasiri kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.
Matei alisema kati ya waliofariki kwa kula muhogo unaosadikiwa kuwa una sumu, wawili ni pacha wakati na wengine wawili wamenusurika na mmoja akiwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Waliofariki katika tukio hilo ni Omary Mohamed na pacha wake Hamis Mohamed na Daud Herman na walionusurika kifo ni Amos Kunambi (30), mkazi wa Kauzeni aliyetibiwa na kuruhusiwa baada ya hali yake kuwa nzuri wakati Joshua Msiani (24) anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa.
Mmoja wa manusura, Joshua Msiani aliwaambia waandishi wa habari hospitalini kuwa walikula mihogo hiyo iliyokuwa imechemshwa wakati wakifyatua matofali eneo la kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.

clouds stream